Tuesday, 29 January 2019

Zingatia haya Unapoanza Kuwekeza katika Hisa

Habari ndugu msomaji wa mtanadao huu wa Wekeza Mtanzania. Tunasema asante mungu kwa siku nyingine, vile vile asante ndugu msomaji kwa kuendelea kutembelea mtandao huu. Bila wewe msomaji sisi hatuna cha kujivunia katika kazi yetu ya uandishi.

Zingatia haya unapoanza kuwekeza 


Karibu tena ndugu msomaji katika somo letu la leo kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanya uwekezaji katika hisa.. Ni muhimu kupata kuyafahamu mambo muhimu na ya msingi ili safari ya mafanikio na uhuru wa kifedha iwe ya uhakika na yenye mafanikio makubwa.

Nipende kukumbusha kuwa kabla hatujaangalia mambo muhimu kuzingatia katika safari ya kuanza kuwekeza ni muhimu ukaweka malengo ya muda mrefu ili kufikia uhuru wa kifedha wa uhakika. Na kama haujaanza kuwekeza katika hisa, nakushauri uanze sasa, huu ndio uwekezaji ambao utakuhakikisshia kipatoa cha uhakika baada ya nguvu ulizonazo leo kupungua, na ndio uwekezaji ambao unakupa uhuru wa kufanya shughuli nyingine bila usimamizi wa karibu sana.

unataka-kuwekeza-katika-hisa-soko-la hisa na haujui uanzie wapi

Mambo haya muhimu kuzingatia unapoanza safari kuwekeza katika hisa

1. Chagua mshauri atakayekuongoza
Ukitaka kufanya jambo lolote kwa ubora na matokeo mazuri, Ni muhimu ukachugua mtu wa kukuongoza ambaye ameshafanya Fanya jambo hilo kwa ubora au mwenye taaluma husika. Kabla ya kuanza uwekezaji wako ni vyema ukachagua mshauri ambaye ni mtandao huu wa uwekezaji na Mtanzania kwa kusoma makala zetu, na ikiwa utahitaji ushauri zaidi toka kwa mwandishi unakaribishwa ila kwa Malipo. 

2. Fuatilia uwekezaji wako
Uwekezaji katika hisa unahitaji ufuatiliaji Kama biashara nyingine hasa kuangalia mwenendo wa bei na ufanyaji kazi wa kampuni ambazo umewekeza. Hii inakusaidia kujua kampuni ambazo umewekeza ambazo zinafanya vizur sokoni. Na pia itakusaidia kujua ni muda sahihi wa kuuza au kununua hisa katika soko.

faida-aipatayo-mwekezaji-kuwekeza katika Hisa

3. Uwekezaji upi wa kuepuka
Kama mwekezaji unatakiwa kuwa na tahadhari ili kupunguza hatari ya kupoteza pesa yako ukiwa unafanya uwekezaji katika hisa. Hatari mojawapo ya kuzingatia hasa unapochagua kampuni ya kuwekeza, usichague kampuni kwa sababu sokoni hisa zake zinauzwa bei ya chini. Nunua hisa kwenye kampuni ambayo ina rekodi nzuri ya mapato, Faida na yenye malengo mazuri. 

4. Kiasi gani cha pesa kinahitajika ili uanze kuwekeza
Watu wengi wakisikia kuhusu uwekezaji, mawazo yao wanahisi inahitajika kiasi kikubwa cha pesa ili uanze kuwekeza katika hisa. Kuwekeza katika hisa hauhitaji pesa nyingi ili uanze kuwekeza, utahitaji kiasi cha shilingi 30,000/= tu au zaidi na utaanza kuwekeza katika soko la hisa na kuanza kuwa mmiliki wa baadhi ya kampuni. Unahitaji kuwa na subira na kuwa na utaratibu wa kununua hisa mara kwa Mara. Ikiwa utakuwa na mtaji wa shilingi 30,000/= hadi 200,000/= nunua hisa kwenye kampuni moja utaongeza uwekezaji wako kwenye kampuni nyingine.  Na ikiwa una mtaji wa shilingi 500,000/= au zaidi wekeza kwenye kampuni mbili au zaidi katika kampuni tofauti.

umuhimu-wa-mwanafunzi-wa-chuo kujijengea nidhamu ya kuweka akiba

5. Umiliki hisa katika Makampuni mngapi
Katika soko la hisa unaruhusiwa kuwekeza katika Kampuni zaidi ya moja. Muhimu kuchagua kampuni ambazo zinafanya vizuri katika mauzo, faida na katika soko. Kwa kuanza nakushauri uanze kuwekeza kwenye tatu, baada ya kufahamu mambo mengi zaidi katika uwekezaji unaweza kuongeza kampuni zaidi za kuwekeza. Ila kumbuka kuzingatia na kiasi cha mtaji ambacho unacho Kama nilivyoelekeza katika maelezo hapo juu. 

6. Vitabu gani muhimu kusoma
Mafanikio = Maarifa sahihi +Muda + Uvumilivu. Ili uweze kufanikiwa katika uwekezaji au katika jambo lolote ni muhimu ukawa na maarifa na taarifa sahihi ambazo zitakusaidia katika kufanya maamuzi sahihi. Kama ni msomaji wa makala katika mtandao huu wa uwekezaji na mtanzania natumai unapata maarifa sahihi ya kukuwezesha kufanya uwekezaji ulio mzuri, ila unaweza kuongeza ujuzi zaidi kwa kusoma vitabu, majarida na nakala zozote ambazo zitaongeza zaidi uelewa wako katika kuwekeza katika hisa. 

7. Zingatia kuwekeza katika Kampuni bora usiwekeze kwenye Kampuni nyingi
Unaweza kufikiri kuwekeza au kununua hisa kwenye kampuni nyingi ndio itakusaidia kufanya vizuri. Unatakiwa kuchagua kampuni bora ambazo zinafanya vizuri sokoni kuliko zingine na sio kuwekeza katika kampuni nyingi. Unaweza kuwekeza tano au tatu tofauti na ukajenga uwekezaji ulio Nora zaidi. 

Nikutakie wakati mwema, na kukaribisha kuendelea kujifunza zaidi kupitia makala zangu

Ukihitaji Ushauri au Maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana kwa Namba 0714 445510 Ila kwa malipo ya shilingi 10,000/=

Emmanuel Mahundi
Wekeza Mtanzania

3 comments:

  1. Ahsante sana kwa wakala yako naitaji kujua zaidi

    ReplyDelete
  2. Tuwasiliane kwa mawasiliano yangu nilioacha kwenye makala

    ReplyDelete
  3. elimu nzuri kaka nitalipia ili nipate maarifa zaidi

    ReplyDelete