Friday, 19 January 2018

Mambo Muhimu kuyafahamu unapowekeza mara ya Kwanza katika HISA

Hakuna muda mzuri wa kuwekeza kama sasa

Inawachukua muda mrefu kwa watu kuchukua hatua kwa ajili ya kuanza kuwekeza katika hisa. Ila hakuna muda sahihi wa kuanza kuwekeza katika hisa kama sasa. Watu wengi wanakuwa waoga kuanza kuwekeza kwa kuhofia kutokuwa na uzoefu katika kuwekeza na kuweza kufanikiwa. Ila nikuambie ndugu msomaji wa makala hii hakuna muda mzuri wa kuanza kuwekeza kama sasa, kama sababu ya kushindwa kuwekeza ni uzoefu ondoa shaka.

Wekeza Hisa kwa mara ya Kwanza


Hakuna uzoefu mzuri kama wa kuanza kufanya jambo ndipo unapojifunza na kupata uzoefu na kuweza kufanikiwa. Hautakiwi kusubiri hadi upate kazi ya ndoto yako au uwe na pesa nyingi au hadi ufikie umri fulani ndio muda wako sahihi wa wewe kuanza kuwekeza na wala sio hadi ufanye maandalizi makubwa ili na wewe uanze kuwekeza, kitu cha muhimu anza sasa kuwekeza.


Kitu cha kwanza kuanza kufanya unapotaka kuwekeza

Kitu cha muhimu kwa mwekezaji anayetaka kuanza kuwekeza kukifahamu, ni muhimu ukamtafuta dalali/broker wa soko la hisa. Makampuni ya madalali soko la ndio wanaunganisha wauzaji na wanunuzi wa hisa katika soko la hisa.

Katika kuchagua dalali ni vyema ukatafuta madalali ambao wanaweza kukushauri ni uwekezaji upi unatija zaidi, ni muhimu kuchagua mshauri ambaye anaweza kukupatia taarifa sahihi kuhusu uwekezaji katika soko la hisa.

Ni muhimu kupata mwongozo ambao utakusaidia kujua mawakala wa soko la hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE). Mwongozo utakusaidia kujua kila hatua ambazo mwekezaji anatakiwa kupitia anapohitaji kununua hisa. Vile vile ni muhimu ukafahamu kampuni ambazo zinafanya vizuri katika soko la hisa ili uwekeze katika kampuni ambazo zitakuza uwekezaji wako.

Kujua Kampuni ambazo zinafanya vizuri soma maelezo haya

KUPATA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA FEDHA ZA KAMPUNI KATIKA SOKO LA HISA

Sekta ya Huduma (Commercial services) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji (Finance, Banking and Investment) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Viwanda (Industrial) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Madini (Mining) na Mawasiliano (Telecom) kwa pamoja unapata kwa Tsh 10,000

Ikiwa utahitaji kupata Uchambuzi kwa sekta zote kwa pamoja utalipia Tsh 30,000 badala ya kulipia Tsh 40,000.

Malipo unafanya kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako

Aina gani ya uwekezaji ambao sio mzuri?

Watu wengi ambao nimekuwa nawasiliana nao wamekuwa wakiniuliza ni hisa gani zinauzwa bei ya chini, na wakiwa na lengo la kutaka kununua hisa za kampuni ambazo zinauzwa kwa bei ya chini. Ila nakushauri usifanye kosa hili usinunue hisa za kampuni kwa sababu zinapatikana kwa bei ya chini (cheap). Hakuna uhusiano wowote kati ya hisa ambazo zinauzwa kwa bei ya chini na ukuaji wa uwekezaji wako.

Unachotakiwa mwekezaji kuwekeza kwenye kampuni ambayo ni bora na inafanya vizuri katika taarifa zake za fedha na ipo katika mtiririko wa kuendelea kufanya vizuri zaidi. Watu wengi hawana ujuzi wa kutambua ni kampuni gani inafanya vizuri katika taarifa zake, basi nimekuandalia uchambuzi wa taarifa za fedha ambazo utaweza kujua ni kampuni gani ipo vizuri zaidi. Maelezo jinsi ya kupata uchambuizi yapo hapo juu yameandikwa kwa rangi nyekundu.

Nahitaji kiasi gani nianze kuwekeza ?

Swala la kiasi cha kuanza kuwekeza katika hisa nalo limekuwa ni kikwazo kwa watu wengi ambao wamekuwa wakitamani kutaka kuanza kuwekeza. Basi nikuambie ndugu msomaji hauihitaji mamilioni ya pesa kuanza kuwekeza katika hisa, unaweza kuanza na kiasi kidogo jinsi ambavyo utazoea ndivyo utakavyo ongeza zaidi uwekezaji wako.

Unaweza kuanza kununua hisa zenye thamani ya shilingi 30,000 kwa kila mwezi au zaidi. Jinsi ambavyo utakuwa makini na mpango wako wa uwekezaji wako ndivyo utakavo ongeza kiasi cha uwekezaji wako na kuweza kutawanya uwekezaji wako katika kampuni tofauti.

Naweza kuwekeza kwenye kampuni ngapi katika soko la hisa?

Nakushauri kama ni mgeni na una kiasi cha chini ya laki moja ni vyema ukaanza na kampuni moja ya kuwekeza katika soko la hisa ila baada ya miezi miwili unaweza kuongeza hisa kwa kununua kwenye kampuni nyingine ambayo utaona inafaa kwa ajili ya kukuza uwekezaji wako.

Jinsi utakavyo ongeza kiasi cha kuwekeza au jinsi ambavyo utavyokuwa na utaratibu wa kila mwezi kuweza, ndivyo ambavyo utaongeza idadi ya kampuni tofauti kuwekeza. ukijijengea nidhamu ya uwekezai ndivyo utakavyokuza uwekezaji wako.


Kwa ajili ya kupata Mafunzo zaidi, Uchambuzi wa taarifa, Vitabu vya Uwekezaji. Karibu Ujiunge na Kikundi (Group) la Whatsapp kwa ada ya shilingi 25,000 kwa mwaka mzima.

Emmanuel Mahundi
emmanuelmahundi@gmail.com
Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment