Tuesday, 23 January 2018

HISA: Jinsi ambavyo Utafanikiwa katika Uwekezaji

Hakuna jambo gumu ambalo wawekezaji wengi wanakutana nalo kama kuchagua uwekezaji wa kampuni ambayo inafanya vizuri na itaendelea kufanya vizuri. Na hiki ni kitu muhimu kwa mwekezaji kwa sababu lengo kubwa la mwekezaji ni kuongeza thamani ya uwekezaji wake.

Jinsi ambavyo Utafanikiwa katika Uwekezaji 


Jambo muhimu kwa mwekezaji anapoamua kuwekeza katika hisa ni muhimu kutoendeshwa na hisia katika maamuzi ya kununua na kuuza hisa. Kwa sababu unaweza kuuza hisa zako kwa sababu tu hisa zako zimeshuka kwa asilimia 10% katika kipindi fulani. Kumbe kushuka kwa hisa zako ni mzunguko tu wa muda hasa pale taasisi kubwa zinapouza hisa kwa wingi katika soko.

Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kusababisha kushindwa kufanikiwa katika uwekezaji wa hisa ila muhimu kufahamu vitu hivi ambavyo vitaongeza nafasi ya ushindi katika uwekezaji wako katika soko la hisa


Kupata Pesa nyingi ni Muhimu ukanunua hisa katika Kampuni bora na katika kipindi sahihi

Ili mwekezaji uweze kutengeneza pesa nyingi katika uwekezaji wako ni muhimu kununua hisa katika kampuni bora. Kampuni bora ni kampuni ambayo inafanya vizuri katikauendeshaji wake na vile vile inamatarijio ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Unawezaje kujua kampuni hii ni bora

Tunafahamu kampuni bora toka katika taarifa zake za fedha kwa kufanya uchambuzi wa taarifa za fedha za Kampuni (Tuna angalia mauzo ya kampuni, Faida ya kampuni, uwezo wa kutumia rasilimali za kampuni n.k)

Ni muhimu kununua hisa kwenye kampuni bora katika kipindi sahihi, mfano kipindi ambacho kampuni inauza hisa zake kwa mara kwanza (IPO) hapa mara nyingi hisa huuuzwa chini ya thamani hali ya kampuni kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji.
 Angalizo usinunue hisa kwa kila kampuni ambayo inauzwa hisa zake kwa mara ya kwanza, muhimu kusoma taarifa muhimu za kampuni kabla ya kununua hisa.

Angalia kampuni ambayo ina mauzo makubwa (sales) na mapato kwa mwekezaji ni makubwa (earnings per share)

Mauzo ya Kampuni ni kipimo cha kampuni katika kufanya vizuri katika soko na sekta husika. Utatambua mauzo ya kampuni kwa kusoma katika taarifa za fedha za kampuni husika na kujua kwa kiwango gani kampuni imeweza kupata mauzo ya kutosha. Hata kwa biashara ndogo, ikiwa biashara ina mauzo makubwa ni kipimo cha kuonyesha biashara hiyo ina mzunguko mkubwa katika soko.

Kama mwekezaji ni muhimu kuangalia kampuni yenye mauzo makubwa na ambayo ina kipato zaidi kwa wawekezaji (EPS). Kwa sababu kipato kwa mwekezaji ni kipimo cha kampuni kutengeneza faida ya kutosha kwa wawekezaji.


Angalia Kampuni ambayo inatoa mapato makubwa kwa wanahisa (ROE)

Kama ilivyo kwa mfanyabiashara atachagua biashara ambayo ana uhakika itampatia faida ya kutosha na kuweza kurudisha mtaji wake. Hata katika uwekezaji katika hisa ni muhimu kwa mwekezaji kuwekeza katika kampuni ambayo inatoa mapato makubwa kwa mwekezaji. Mapato hayo ndio kiashiria cha utumiaji vizuri wa rasilimali za kampuni, pia ndio mapato ambayo mwekezaji anapata baada ya pesa yake kuwekeza katika mtaji wa kampuni husika.

Kama unataka kuwekeza kwenye kampuni yoyote angali (ROE) ambayo ina anzia kwa asilimia 15% au zaidi ya hiyo.

KUPATA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA FEDHA ZA KAMPUNI 

Sekta ya Huduma (Commercial services) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji (Finance, Banking and Investment) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Viwanda (Industrial) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Madini (Mining) na Mawasiliano (Telecom) kwa pamoja unapata kwa Tsh 10,000

Ikiwa utahitaji kupata Uchambuzi kwa sekta zote kwa pamoja utalipia Tsh 30,000 badala ya kulipia Tsh 40,000.

Malipo unafanya kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako.

Angalia mzunguko wa bei katika soko

Ili mwekezaji inatakiwa kuwa makini katika kipindi cha kununua ili iweze kutengeneza faida ya kutosha katika hisa. Nunua hisa bei ikiwa katika ambacho ina anza kupanda, katika kipindi hiki mwekezaji anakuwa na uhakika wa uwekezaji wake kukua katika kipindi kifupi cha uwekezaji wake. Nawezaje kujua bei ina karibia kupanda ? Ili uweze kufanikiwa kwa kutumia mbinu hii unatakiwa kuwa na utamaduni wa kufuatilia mabadiliko ya bei kwa kampuni ambazo umechagua kuwekeza, katika kufuatilia mabadiliko hayo unaweza kujua bei zimeshuka na kwa muda huo zimeanza kuongezeka.

Asante kwa kuendelea kuwa Msomaji wa blog hii

Emmanuel Mahundi
emmanuelmahundi@gmail.com

Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment