Wednesday, 12 April 2017

Umuhimu wa Mwanafunzi wa Chuo kujijengea Nidhamu ya kuweka Akiba

Karibu ndugu Msomaji wa Mtandao huu wa Uwekezaji na Mtanzania. Kuendelea kujifunza vitu vingi kuhusu fursa, taarifa na mbinu mbalimbali kuhusu Uwekezaji katika soko la Hisa. Katika Makala ya leo Tutajifunza umuhimu wa Mwanafunzi wa Chuo au mtu yeyote wa kujiwekea akiba na kuwekeza.

Ili uweze kuwekeza katika hisa unahitajika kuwa na kiasi cha fedha ambacho utanunua hisa za Kampuni na kufanya uwekezaji wako. Hii inamaanisha ili uwekeze unatakiwa kuwa na kiasi ambacho umewekea akiba au kipato ambacho umepata kwa njia yoyote. Mfumo wa kujiwekea akiba kwa mwanachuo na kuwekeza ni utaratibu ambao una muandaa kijana toka katika lika la chini kuwa na nidhamu ya fedha na kukuza thamani ya akiba yake.

Kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa kwa mwanafunzi kujijengea utaratibu wa kujiwekea akiba kwa zile pesa ndogo ambazo anazipata kama fedha ya kujikimu akiwa shuleni. dhamu hii ya kujiwekea akiba inamtengenezea njia bora ya kuweza kuwekeza na kujishughulisha katika ujasiriamali mbali mbali na kujiingizia kipato
Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment