Monday, 17 April 2017

Faida aipatayo Mwekezaji kuwekeza katika HISA

Karibu ndugu wasomaji wa mtandao huu wa uwekezaji na Mtanzania katika mfululizo wa makala za kukuelimisha na kukuabarisha kuhusu uwekezaji katika hisa. Leo tutaangalia faida ambazo mwekezaji atazipata kama atawekeza pesa yake katika hisa. Kama ambavyo tunajua kuwa hakuna biashara ambayo haina changamoto katika ulimwengu huu ila tupate kujifunza kuhusu faida ambazo mwekezaji atazipata ikiwa atachagua uwekezaji katika Hisa.

Faida ya Kununua Hisa


Faida za kuwekeza katika hisa kama zifuatazo

Mwekezaji atanufaika na ukuaji wa Uchumi
Watu wengi tumekuwa tukilalamika kuwa uchumi wa nchi unakua ila sisi maisha yetu bado yapo vile vile. Na hata tunaposikia sekta ya viwanda au mawasiliano imekuwa bado tunaona haituhusu kabisa katika Maisha yetu. Ila kama utawekeza pesa yako kwenye Kampuni tofauti na uchumi ukakua katika sekta hizo, pia na wewe mwekezaji pesa yako inakua. Kwa hiyo kama mwekezaji utanufaika na ukuaji wa uchumi wa nchi yako.

Ni rahisi kununua Hisa
Unaweza kununua hisa kupitia kwa mawakala wa soko la hisa (Madalali), kwa kutembelea ofisi za mawakala hao au unaweza kununua hisa kwa madalali wa soko la hisa online ukiwa popote pale Tanzania. Urahisi huu wa ununuzi na uuzaji wa hisa, unafanya uwekezaji katika hisa kuwa wa kipee na rahisi kufanywa na mtu yoyote.

Unatengeneza pesa kwa njia mbili tofauti
Wawekezaji wengi wanapenda kununua hisa katika bei ndogo na kuuza kwa bei kubwa au kuna wengine ambao wanapenda kununua hisa kwenye Kampuni ambayo thamani yake inakua kwa kasi katika soko na ufanisi wake. Wawekezaji wa namna hii wanatengeneza faida katika kipindi kifupi na wanategeemea Kampuni kufanya vizuri katika kipindi kirefu. Vile vile kuna wawekezaji ambao wanawekeza kwenye kampuni ambayo inatoa gawio kwa wamiliki wa hisa.

Ni rahisi kuuza Hisa
Kama ambavyo ni rahisi kununua hisa na hata kama utakuwa unahitaji kuuuza hisa zako utawasiliana na mawakala(Dalali) wa soko la hisa kwa ajili ya kuuza hisa zako. Faida unaweza kuuza hisa zako muda wowote ule.


Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment