Wednesday, 14 January 2015

#Kuanzisha Biashara: Mambo ya msingi kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara mpya.Watu wengi wamekuwa wakitamani kumiliki na kuendesha biashara zao ili kujiongezea kipatao, kutengeneza ajira au kujiajiri. Kutokana na kuongeza kwa fursa nyingi katika sekta ya biashara, watu wengi wametamani kumiliki na kuendesha biashara zao. Ili biashara iwe ya mafanikio kuna taratibu na kanuni za kufuata ili ufanikiwe katika biashara hiyo.
Hivi ni vitu vya msingi kwa mfanyabiashara kuvifahamu kabla ya kuanzisha biashara.

Kufahamu mahitaji ya wateja wako
Kama mfanyabiashara ni vizuri kufahamu mahitaji ya wateja katika eneo lako, kupitia mahitaji halisi ya mteja basi kuna fursa ya wewe kuanzisha biashara. Mfano kama eneo Fulani Car Wash zote zinafungwa ikifika jioni, wewe unaweza kuanzisha Car Wash ambayo inatoa huduma katika kipindi cha jioni.

Kufahamu ni sehemu gani biashara yako inatakiwa
Sio kila biashara inafaa kila mahali, kwa hiyo kama mjasiriamali ni vizuri ukatambua mahali ambapo biashara yako itafaa kutokana na mahitaji husika ya wateja. Kuna aina za biashara ambazo zinafaa kuwepo katika barabara kuu na nyingine katika mkusanyiko wa watu. Kama mjasiriamali lazima uweze kutambua biashara yako inafaa kuwepo mahali gani?

Kufahamu kuhusu soko la bidhaa/huduma yako
Kuweza kutambua soko la bidhaa/huduma ni sehemu mojawapo ya kukua na kuimarika kwa biashara yako. Biashara yoyote lazima iwe na wateja wa bidhaa/huduma ili iweze kuwepo katika soko. Kwa hiyo kama mfanyabiashara ni vyema uweze kuwatambua wateja, kuwavutia waweze kupata bidhaa/huduma na kuweza kuwamiliki wateja na waweze kuendelea kuwa wako bila ya kuwapoteza.

Kufahamu mahitaji halisi ya biashara (business facilities)
Mahitaji halisi kama vitendea kazi vya biashara yako ni muhimu kuvifahamu na kujua gharama zake ili uweze kuvipata ambavyo vinaendana na mahitaji halisi na kwa gharama ndogo. Vitu hivi ndio msingi wa utoaji huduma katika biashara yako.

Kuwa na mpango kazi wa biashara yako
Kuwa na mpango kazi katika biashara kuhusu jinsi ya kufanya kazi katika maeneo tofauti ya biashara yako kama vile jinsi gani utatoa huduma, jinsi utafuta masoko na uongozi katika biashara yako.
  
Kufahamu jinsi ya utunzaji wa taarifa za fedha za biashara yako 

“Mali bila daftari hupotea bila habari” kama mfanyabiashara ni lazima uwe na kitabu cha kumbukumbu za taaarifa za fedha kuhusu biashara yako. Taarifa hizi zitakusaidia kujua ufanisi wa biashara yako katika vipindi tofauti na kufahamu ni jinsi uweze kukabiliana na changamoto za biashara yako.

Kuna vitu vingi vya kuzingatia  kabla ya kuanzisha biashara hivi ni kati vitu vya msingi kuvifahamu na kuvifanya kabla ujaanzisha biashara yako.

Nakutakia mafanikioa mema katika maisha yako mwaka 2015
Kwa Ushauri/maelezo zaidi tuma ujumbe mfupi kwa

Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment