Saturday, 5 July 2014

SEHEMU YA KWANZA KATIKA KILIMO CHA UYOGA1. UANDAAJI WA SHAMBA LA UYOGA

Kama nilivyo ahidi katika makala yangu iliyopita kuwa nitaendesha mafunzo kuhusu kilimo cha uyoga na hatua zote muhimu ambazo unatakiwa kuzifuata. Kwanini? Naendesha mafunzo haya ya kilimo cha uyoga.
1
.        Kutokana na kuongeza kwa vijana wengi kukosa ajira.
.       Kwa sababu biashara hii inahitaji mataji mdogo.
.       Ni teknolojia rahisi ambaayo kila mtu anaweza kuifanya.
.       Ni lishe bora kwa mwanadamu

Somo hili litakusaidia kujua hatua zote za kilimo cha uyoga kwa mifano rahisi na picha ili uweze kulifanya bila ya matatizo yoyote. Vilevile somo linajaribu kuonyesha kwa watanzania kuwa kuna biashara ambazo unaweza kufanya ukiwa na mtaji mdogo na kuweza kutengeneza pesa.

MAHITAJI MUHIMU KWA AJILI YA KILIMO CHA UYOGA
1.       Vyumba viwili
2.       Majani makavu ya migomba
3.       Mbegu za uyoga (ziko za aina tofauti)
4.       Chokaa
5.       Sukari
6.       Pipa
7.       Kamba ya katani
8.       Mifuko ya plastiki (kwa ajili ya kuweka mchanganyiko wa majani na mbegu ili kuweza kuotesha uyoga)

Somo litaendelea makala inayofuata ambayo itakueleza kwa picha hatua zote za uandaaji wa shamba lako la uyoga. Usikose fuatilia blog yako UWEKEZAJI NA MTANZANIA kupata vitu vizuri ambavyo vitabadilisha maisha yako na kuondokana na fikra kwamba lazima uajiriwe ili ufanikiwe.

Mwandishi Emmanuel Mahundi
Mawasiliano emmanuelmahundi!@gmail.com
Wekeza Mtanzania

2 comments:

  1. Habari Ndugu Mahundi
    Mimi nimepitia makala yako kwa ajili ya kilimo cha uyoga, asante sana naitaji msada wako zaidi

    ReplyDelete
  2. Nahtaj kuanza kilimo cha uyoga nahtaj msaada wako.Nipo Arusha

    ReplyDelete