Monday, 4 February 2019

Ujumbe wa Leo: Niwekeze kwenye Kampuni Ngapi??

Habari ya siku nyingine ndugu mwekezaji na msomaji wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania. Karibu katika siku nyingine kwa ajili ya kuongeza maarifa katika nyanja ya uwekezaji katika hisa za kampuni zilizo katika soko la hisa (Soko la Hisa la Dar es Salaam).

Kampuni ya kuwekeza


Katika Ujumbe wa leo kwako mwekezaji na msomaji wa mtandao huu, Napenda kuzungumzia kuhusu ni kampuni ngapi unashauri kuwekeza.

Wekeza kwenye Kampuni kubwa na chache, Muhimu kuchagua kampuni kubwa na mara zote kampuni kubwa ndio ambazo zinafanya vizuri. Kampuni kubwa ni ile ambayo inafanya mauzo mazuri, Faida inayoongezeka kila mwaka kwa 20% au zaidi. Katika Kampuni kubwa chagua kampuni tatu hadi sita, ila inategemea kiasi cha mtaji ambacho unacho katika kipindi hicho. Ni muhimu kuwekeza katika hiyo idadi ya kampuni ili iwe rahisi kufuatilia uwekezaji wako ili uweze kutengeneza faida nzuri.

Soma... Kwanini Kampuni inauza hisa zake

Kuna usemi unasema " Unalipwa kutokana na kiasi ambacho umetoa" Katika uwekezaji katika Hisa utalipwa kulingana na thamani unayotoa unapofanya uwekezaji wako. Ukinunua hisa kwa sababu zinauzwa bei ndogo, vile vile utalipwa kwa thamani ndogo au kupoteza kabisa mtaji. Mara zote kampuni kubwa ndizo ambazo zinafanya vizuri sokoni na ndizo ambazo bei zake zipo chini. Kwa hiyo ndugu mwekezaji nakushauri wekeza kwenye Kampuni kubwa na ambayo inafanya vizuri sokoni na katika utendaji wake. Usishawishiwe kununua hisa kwenye kampuni kisa inauzwa katika bei za chini.

Jinsi ambavyo utafanikiwa katika uwekezaji

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi
Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment