Thursday, 7 February 2019

Taarifa ya Fedha DSE ya Robo ya mwisho ya mwaka 2018 (Quarter 4)

Habari ndugu mwekezaji na mdau wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania, karibu tena katika mfululizo wa makala na taarifa ambazo zitaongeza ujuzi na kukupatia nafasi nzuri ya kufanikiwa katika uwekezaji katika hisa.

Taarifa ya Robo mwaka DSE


Leo nina habari njema kwako mwekezaji kukupatia uchambuzi kuhusu Kampuni ya Dar es slaam Stock Exchange (DSE) ambayo pia ipo katika soko la hisa. Taarifa hizi zinahusu kuhusu utendaji wake katika kujiingizia kipato, Matumizi, Faida na kuhusu gawio.

Nitaeleza kwa uchache ila katika vipengele muhimu ambavyo vitakupa mwanga kuhusu utendaji wa Kampuni hii ambayo ndiyo inahusika katika kusimamia shughuli zote za ununuaji na uuzaji wa hisa, pia ndio inayozisajili kampuni katika soko.


Uchambuzi wa Kampuni ya Dar es salaam Sock Exchange (DSE) katika Vipengele

1. Mapato (Revenue)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa disemba 2018 Kampuni ya DSE imeweza kutengeneza mapato ya bilioni (1,529,451,170) ukilinganisha na mapato ambayo ilitengeneza katika robo ya tatu ya septemba mwaka 2018 kwa kiasi cha shilingi bilioni (1,319,392,701). Mapato ya robo ya nne mwezi disemba yameongezeka kwa zaidi ya milioni mia mbili, sawa na asilimia kumi na tano (15.92%). Na hii ni ishara nzuri katika utendaji wa kampuni.

Kwanini Kampuni inauza Hisa Zake

2. Faida Baada ya Kodi (Profit after tax)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa disemba 2018, Kampuni ya DSE imeweza kutengeneza kiasi cha faida ya shilingi milioni mia tatu (307,729,168) ukilinganisha na faida ambayo ilitengeneza katika robo ya tatu ya septemba mwaka 2018 kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja (134,698,081). Faida ya robo ya nne ya mwezi disemba imeongezeka kwa zaidi ya milioni mia moja na sabini, sawa na ongezeko la faida kwa asilimia 128.5% kutoka kwenye faida ya robo mwaka ya tatu.

3. Kipato cha Kila Hisa (Earning per Share)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa mwezi disemba 2018, kampuni imeweza kutengeneza mapato ya kila hisa moja ya shilingi 13 ukilinganisha na mapato ya robo ya tatu mwaka 2018 ya shilingi 6 kwa kila hisa moja. Katika robo mwaka wa nne mapato kwa kila hisa yameongezeka kwa kiasi kikubwa sawa na asilimia 116.7% toka kwenye mapato kwa kila hisa ya robo tatu ya mwaka 2018.

Zingatia haya unapoanza Kuwekeza katika Hisa

Ili kuweza kusoma taarifa nzima ya robo ya nne ya mwaka 2018 bonyeza maandishi hapo chini na kuweza kupakua taarifa nzima.

Pakua taarifa na Kuisoma kwa kubonyeza linki hii
Link Download Unaudited financial statement quarter ended december

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment