Sunday, 10 February 2019

Nunua Hisa kwenye Kampuni Hizi

Habari ndugu msomaji wa makala hizi za Wekeza Mtanzania, karibu tena upate kuongeza maarifa sahihi kuhusu uwekezaji katika hisa. Ndugu msomaji umeshaanza kuwekeza katika hisa? Ikiwa umeanza kuwekeza ' Hongera Sana'. Kama bado haujaanza kuwekeza katika hisa nakushauri uanze sasa. Na ikiwa haujui uanzie wapi Nitafute kwa namba hapo chini mwisho wa makala hii nikuelekeze.

Nunua hisa


Karibu katika makala ya leo tutadodosa kuhusu ni kampuni gani amabazo unaweza kuanza kuwekeza katika hisa na kujenga uwekezaji imara na wenye manufaa kwako mwekezaji. Kampuni ambazo zipo katika soko la hisa zinatofautiana ubora kutoka kampuni moja hadi nyingine. Kwa hiyo kazi yako mwekezaji ni kuchagua kampuni bora kuwekeza na kuendelea kujenga uwekezaji wako huku ukiwa unaendelea kupata gawio.

Baadhi ya wawekezaji wanapenda kununua hisa kwenye kampuni ambazo thamani yake ni sawa na thamani ambayo ipo sokoni. Baadhi ya wawekezaji upendelea kununua hisa kwenye kampuni ambazo bei zake zipo chini ya samani halisi ya kampuni (Mfano hisa za kampuni sokoni zinauzwa Shilingi 1000 ila thamani halisi ya hisa ni shilingi 2500), mwekezaji atanunua akiwa na lengo kuwa bei zitaongezeka kufikia thamani halisi. Ila mimi nakushauri ununue kwenye kampuni ambazo zinakua na ambazo bei ya sokoni ina akisi thamani ya hisa ya kampuni husika. 

Siku ya keo ndugu msomaji mpendwa nitakujuza sifa nzuri za Kampuni ambazo unatakiwa uweke mtaji wako (kununua hisa) ili uweze kufanya uwekezaji mzuri.

Chagua Kampuni ya kuwekeza katika Sekta zinazofanya vizuri. Mwekezaji unapotoa mtaji wako na kuwekeza lengo ni kukuza mtaji ili uweze kujitengenezea faida. Na ili uweze kutengeneza faida katika uwekezaji katika soko La hisa, ni muhimu kwako kuwekeza katika sekta ambazo zinafanya vizuri sokoni. Na utajuaje sekta Huduma au viwanda inafanya vizuri, ni kwa kupitia kusoma taarifa za kampuni pia na ufanisi wa kampuni hizo katika soko la hisa na kupata taarifa kuhsu utendaji wa kampuni husika.

Sekta ya Viwanda, Uwekezaji na Sekta ya Mabenki na Fedha, ndizo zinafanya vizuri sokoni (Katika soko la hisa la Dar es salaam) ukilinganisha na sekta nyingine. Pamoja kwamba nimeeleza kuwa sekta hizo zinafanya vizuri sio makampuni yote katika hizo sekta yanafanya vizuri. Kama mwekezaji unatakiwa kufanya uchunguzi kwa kila sekta ili uweze kuchagua kampuni nzuri ya kuwekeza ili kukuza uwekezaji wako.

Kwa kusoma taarifa za fedha za kampuni na kufuatilia mafanikio ya kampuni husika sokoni, Itakusaidia kuchagua kampuni nzuri. Kama nilivyoeleza mwanzo kuwa wekeza katika sekta inayofanya vizuri, na katika kila sekta chagua kampuni ambazo zinafanya vizuri katika sekta husika (Unachagua bora zaidi katika sekta hiyo) ili kufanya uwekezaji bora.

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi
Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment