Wednesday, 30 January 2019

Ujumbe: Wekeza kwenye Kampuni Kubwa

Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania, karibu tena katika siku nyingine katika safari ya kuongeza maarifa ili kuweza kufanya uwekezaji bora na kuongeza kipato. Katika siku ya leo nina ujumbe kwako mwekezaji katika hisa kuhusu kuchagua kampuni ya kuwekeza. Na kama bado haujanza kuwekeza nakushauri uanze mapema ili uanze kuongeza thamani ya uwekezaji wako.

Wekeza kwenye Kampuni kubwa


Kama nilivyoeleza hapo juu, leo nitazungumzia kuhusu kuchagua kampuni ya kuwekeza katika soko la hisa. Katika soko kuna Kmapuni zaidi ya ishiri, na kampuni zote zinauzwa bei tofauti vile vile zina thamani tofauti.

Ushauri wangu kwako mwekezaji kabla haujanunua hisa zingatia haya machache kuhusu kuwekeza katika hisa;

Usinunue hisa kwa sababu zinauzwa bei ndogo
Ndugu mwekezaji unapohitaji kununua hisa, usiangalie kwa sababu kampuni inauza hisa zake katika bei ndogo ambayo itakufanya upate hisa nyingi. Utapoteza mtaji wako ikiwa utazingatia udogo wa bei iliyo sokoni. Nunua hisa kwenye kampuni Kubwa na mara nyingi zinauzwa katika bei kubwa, ila sio kampuni zote zenye bei kubwa ni nzuri.

Zingatia haya unapoanza kuwekeza katika hisa

Kampuni kubwa ina sifa zifuatazo ndugu msomaji/mwekezaji Ina mauzo mazuri ya bidhaa/huduma, Inatengeneza faida nzuri, Inatoa gawio wa wawekezaji, Ina uongozi mzuri na mipango mizuri ya bidhaa/huduma zake katika kipindi kijacho. Kwa kifupi ni kampuni ambayo inajiendesha kwa kutengeneza faida na pia inafanya vizuri sokoni (Soko la Hisa).

Soma hii.. Jinsi ya kuchagua Uwekezaji unaokua

Natumai kwa haya machache umefahamu kuhusu utaratibu mzuri wa kuchagua kampuni unapohitaji kuwekeza katika hisa.

Asante na endelea kutembele mtandao huu usisahu kulike ukurasa wetu wa Facebook na kupakua app kwenye matangazo ya pembeni.

Kazi Njema

Kwa ushauri au ufafanuzi zaidi tuwasiliane kwa 0714 445510 ila utachangia shilingi 10,000 kwa tigo pesa.

Emmanuel Mahundi Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment