Tuesday, 2 May 2017

Jinsi ya Kuchagua Uwekezaji Unaokua katika Hisa

Karibu ndugu wasomaji wa mtandao huu wa uwekezaji na Mtanzania katika mfululizo wa makala za kukuelimisha na kukuhabarisha kuhusu uwekezaji katika hisa. Leo tuta angalia jinsi mwekezaji ambavyo anaweza kuchagua uwekezaji ambao unakua katika Hisa na kuweza kujiongezea kipato na kukuza uwekezaji wake.Katika somo la leo utapata kujifunza kujifunza mwongoz ambao utakupa mwanga jinsi ya kuchagua Kampuni nzuri ya kuwekeza. Maswali ya kujiuliza kabla haujachagua Kampuni ya kuwekeza katika soko la Hisa.

Kampuni ina historia nzuri ya kukua katika Kipindi cha Nyuma
Je Kampuni unayotaka kuwekeza ina historia ya kukua katika mapato, faida kwa miaka mitano au zaidi katika kipindi cha nyuma. Earning per share(Kiasi cha kila hisa ambacho kinapata) kinakua kwa kila mwaka na katika kiwango kizuri. Ukuaji huu wa Kampuni katika sehemu tofauti katika kipindi cha nyuma kunatupa picha halisi ya ufanisi wa Kampuni husika. Na kumshawishi mwekezaji kuwekeza katika Kampuni hii.

Ukuaji wa Kampuni katika Kipindi kijacho
Kama mwekezaji ni vyema kutambua kuwa Kampuni ambayo unataka kuwekeza itaweza kukua katika kipindi kijacho. Kujua kufanya vizuri kwa Kampuni katika kipindi kijacho kunatokana na ufanisi wa Kampuni katika kipindi hiki na mipango mizuri ya baadae ya kampuni. Japo kufanya uchambuzi unahitaji kuwa na ujuzi kiasi katika kusoma taarifa za fedha za Kampuni husika.

Uimara wa Uongozi wa Kampuni
Je uongozi wa kampuni unafanya vizuri kulingana na mali za Kampuni zinazomiliki? Au kulingana na fursa ya Kampuni katika Soko? Kama Kampuni haifanyi vizuri ila ina mali za kutosha na fursa katika soko ni kubwa, basi uongozi utakuwa na tatizo. Kwa hiyo ni muhimu kwa mwekezaji kupima uongozi kwa kuangalia ufainsi wake katika kutumia mali za kampuni katika kuongeza poto la kampuni.

Uongozi wa Kampuni unaweza kujiimarisha katika Mauzo
Je kampuni ukuaji wake kipato unaendana na ukuaji kipato cha mwanahisa? Je ukuaji wa Kampuni katika kipato ni wa kuridhisha? Kama mwekezaji vyema ukapima hivi vitu kwa uangalifu ili uweze kuchagua Kampuni iliyobora kabisa kwa ufanisi wa uwekezaji wako.

Bei ya Hisa ya Kampuni inakua kwa Kiwango kinachoridhisha
Kama mwekezaji ni vyema uka angali ukuaji wa bei ya Kampuni katika kipindi cha nyuma na kujua kama Kampuni bei ya hisa zake inaweza kukua katika miaka mitatu au zaidi katika kipindi kijacho.


Emmanuel Mahundi
emmanuelmahundi@gmail.com
0714 445510


Wekeza Mtanzania

No comments:

Post a Comment