Saturday, 12 July 2014

HII NDIO NJIA RAHISI AMBAYO UNAWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARALeo tutaangalia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa kutumia njia rahisi. Na jinsi gani unaweza kuzalisha kuku chotara. Kuku chotara ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kabla hatujangalia hatua muhimu za kuzalisha kuku chotara, tutaangalia faida za kuku chotara kwa mwekezaji/mjasiriamali.

Faida za kuku chotara kwa mfugaji na mlaji
Ukuaji mzuri
Nyama  yake ina ladha nzuri na laini
n.k

Hawa ni kati ya kuku chotara ambao ninafuga

HATUA MUHIMU KATIKA UZALISHAJI WA KUKU CHOTARA

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe  lina pitisha hewa ya kutosha na kama unataka kufahamu kwa undani kuhusu maandalizi muhimu ya banda lako. Makala hiyo itakuja kupitia blog yako ya uwekezaji na mtanzania.

Hatua ya pil,i andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.

KUPATA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA FEDHA ZA KAMPUNI KATIKA SOKO LA HISA

Sekta ya Huduma (Commercial services) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji (Finance, Banking and Investment) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Viwanda (Industrial) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Madini (Mining) na Mawasiliano (Telecom) kwa pamoja unapata kwa Tsh 10,000

Ikiwa utahitaji kupata Uchambuzi kwa sekta zote kwa pamoja utalipia Tsh 30,000 badala ya kulipia Tsh 40,000.


Malipo unafanya kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako

Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa
Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji
Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji
KUMBUKA
Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu

Wekeza Mtanzania

1 comment: