Wednesday, 25 June 2014

HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?


Tatizo la ajira limeendea kuwa kikwazo kikubwa cha wahitimu wengi wanaomaliza masomo yao katika ngazi mbalimbali hapa nchini na hata kwa wale ambao hakufanikiwa kuendelea na masomo. Huku sekta ambayo inatoa ajira nyingi kwa wahitimu ni sekta binafsi. JE WE KIJANA UNAKUBALIANA NA TATIZO LA KUKOSA AJIRA HUKU UKISUBIRI SERIKALI?
Suluhisho la tatizo lako liko hapa ndugu, unaweza kujiari kwa mtaji mdogo na ukatengeneza pesa. Nadhani utajiuliza ni biashara gani au ni shughli ipi ambayo inaweza kukuingizia kipato kwa mtaji mdogo. KILIMO CHA UYOGA kati ya biashara ambayo hazihitaji mtaji mkubwa, ni kilimo ambacho hakihitaji mtaji mkubwa sana, kwa wewe kijana ambaye una lengo la kutengeneza pesa hili ni kati ya suluhisho linalokufaha. Bei ya kilo ya Uyoga ni kuanzia Shilingi 6,000 mpaka 12,000 kwa kilo, bei zina tofautia kutokana na maeneo
                                                 
HISTORIA FUPI KUHUSU KILIMO CHA UYOGA HAPA TANZANIA
Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga.

MAHITAJI KATIKA KILIMO CHA UYOGA

Kabla ya kuanza kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua, na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza.

Mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi. 


 Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyole na taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI – Tengeru, Arusha). Hata kwenye maduka ya kilimo na mifugo.

Mahitaji mengine
1. Pipa
2. Majani ya migomba
3. Maranda
4. Visado au lailoni
 

Somo hili la kilimo cha uyoga litakuja wiki ijayo kupitia blog yako UWEKEZAJI NA MTANZINIA


 


Wekeza Mtanzania

2 comments:

 1. Hakika ni zao lenye faida kubwa kiafya, kukuza kipato na kutunza mazingira.
  Tangu nimeanza kilimo hiki ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijajuta.Tunauza uyoga mkavu na mbichi, mbegu bora,Tunatoa mafunzo na ushauri,uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya Uyoga.
  Tunapatikana Dar es Salaam.
  Twitter/Instagram/Facebook: Hertu Farms
  Simu: 0783182632/0713600915
  Whatsup: 0757315931

  ReplyDelete
 2. Ni kilimo kizuri, hert farm ndo wananifanya nipate nguvu zaidi. Hertu farm mpo mbali Sana

  ReplyDelete