Monday, 18 February 2019

Mbinu hizi zitakusaidia kuanza Kuweka Akiba Leo

Habari ndugu msomaji wa makala hizi za Wekeza Mtanzania, karibu tena upate kuongeza maarifa sahihi kuhusu uwekezaji katika hisa. Ndugu msomaji umeshaanza kuwekeza katika hisa? Ikiwa umeanza kuwekeza ' Hongera Sana'. Kama bado haujaanza kuwekeza katika hisa nakushauri uanze sasa. Na ikiwa haujui uanzie wapi Nitafute kwa namba hapo chini mwisho wa makala hii nikuelekeze.

Weka akiba


Nimekuwa nikizungumzia kuhusu kuanza kuwekeza, na bado naendelea kukushauri ndugu uanze kuwekeza leo katika kununua hisa za kampuni na uwekezaji katika mifuko ya pamoja. Watu wengi na hata mimi mwenyewe mwanzo nilikuwa nakumbana na changamoto ya kupata pesa ya kuanza kuwekeza. Unaweza kujiuliza nitapata wapi pesa kuanza kuwekeza na ikiwa majukumu ya familia ni mengi au kipato chako ni kidogo. Je upo tayari kushindwa kuanza kuwekeza na kujitengenezea kipato cha baadae kisa tu una majukumu mengi au kipato chako ni kidogo.

Changamoto ya watu wengi kushindwa kujiwekea akiba, imekuwa ikiwakumba watu wengi hasa kwa wale ambao ni waajiriwa katika sekta binafsi na sekta za umma. Baadhi ya sababu ambazo watu wengi wamekutana nazo kuwa na majukumu mengi ya familia kama kulipia watoto ada,chakula,malazi na mahitaji mengi ambayo yanahusu familia pia baadhi wamekuwa na majukumu yanayohusu wazazi, wadogo, ndugu wengine na marafiki.

Changamoto nyingine baadhi yetu tumekuwa tukilalamika kuhusu kupata kipato kidogo katika shughuli zetu za kila siku za ujasiriamali na kwenye ajira rasmi. Waajiriwa wamekuwa wakilalamika kuwa mishahara ni midogo na inawatosha kwa mahitaji ya kula, malazi na mahitaji mengine madogo. Wajasiriamali nao wamekuwa wakilalamika kuwa biashara wanazofanya zimekuwa zikiwatosha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumbani na hata kuishia kwenye madeni.

Soma na hii Nunua hisa kwenye Kampuni hizi

Kwa changamoto zote hizo ambazo zinawakabili watu ambao wameajiriwa na wale ambao wamejiajiri. Je tuendelee kulalamika kila siku na miaka izidi kwenda na mwisho wa siku uzee utukute katika mahangaiko ya kulalamika kuwa kipato chetu ni kidogo na matumizi ni makubwa.

Mimi nasema hapana kwa sababu hata mimi nilikuwa muhanga wa changamoto hiyo ya kulalamika kuwa kipato ni kidogo. Ila baada ya kupata mbinu chache kuhusu pesa nikatambua kuwa pesa niliyonayo japo ni ndogo inatosha kuweka akiba na kuanza kufanya biashara na kuongeza kipato kingine na pesa nyingine kuwekeza ili niwe na uhuru wa kifedha hapo baadae.

Unaweza kujiuliza naweza nikaanza kuweka akiba ikiwa pesa hii niliyona ni ndogo na pia tayari nina madeni mengi ambayo yananikabili. Katika kitabu cha siku nyingi kinaitwa " The Richest Man in Babylon" na baadhi ya vitabu vingine nilivyosoma viliweza kunipatia mbinu ambazo ziliweza kunisaidia kuanza kuweka akiba  na kisha kuanza kufanya biashara na kuwekeza pia kwa kipato changu kilekile. Vile vile vilinipatia njia za kuweza kuanza kupunguza madeni ambayo nadaiwa na mwisho wa siku nilijikuta sina madeni na akiba yangu ikiendelea kukua.

Soma na Hii Kwanini usinunue hisa zinazouzwa bei ndogo

Nawezaje kuanza kuweka akiba leo

1) MFANYAKAZI (Mwajiriwa)
Sehemu kubwa ya waajiriwa wamekuwa wanategemea kipato toka katika mishahara ambayo wamekuwa wakipata kila mwezi. Mwajiri amekuwa akikulipa wewe mfanyakazi kwa gharama ya muda, nguvu na ujuzi ambao umekuwa ukiutoa katika taasisi au kampuni. Je umewahi kujiuliza kuwa umewahi kujilipa wewe mwenyewe baadaya kupata mshahara kabla hujafanya matumizi yoyote?. Je umekuwa na tabia ya kuandika matumizi yako ya kila mwezi?

Mbinu hizi zitakusaidi kuanza kuweka akiba wewe Mwajiriwa na Mfanyabiashara

a) Ukipata mshahara wako au faida ya biashara yako, kabla ya kufanya matumizi yoyote unatakiwa kujilipa asilimia kumi 10% ya mshahara wako na ikiwa itakuwa ngumu unaweza kuanza na asilimia tano na ikiwa utaanza kuweka asilimia kumi natumai utafurahi pale utakapoona sehemu yako ya kumi ikiongezeka kila mwezi. Angalizo sehemu hii ya kumia ambayo utaweka hautakiwi kuitumia kwa matumizi yoyote na nakushauri ukaifungulia akaunti ya muda maalumu (Fixed account) ambayo hautaruhusiwa kuitoa hadi muda ufike.

Nimezungumzia kuhusu kutoitumia hiyo sehemu ya kumi ya kipato chako kwa jambo lolote, kwa sababu matatizo na dharura zipo kila siku tafuta njia nyingine ya kuzitatua na sio kutumia sehemu hiyo ya kumi.

b) Kuwa akaunti ya dharura
Kama ambaovyo nimesema hapo juu sehemu ya kumi hauruhusiwi kuitumia, ila katika kipato chako kile cha mshahara baada ya kutoa sehemu ya kumi kiasi kilichobaki unatakiwa kutenga sehemu ya pesa na kuweka katika akaunti ya dharura (kama vile ugonjwa, msiba na n.k). Akaunti hii inaweza kuweka kuanzia asilimia ishirini au zaidi kutoka katika kipato chako. Na pesa hii itakusaidia katika kutatua dharua zozote ambazo zitatokea ndani ya mwezi huo, kama kuna msiba wa rafiki, ndugu au umepata na dharura ya ugonjwa pesa hii itasaidia kufanikisha kutatua matatizo.

c) Matumizi yote unayofanya yaandikwe
Uwe  na tabia ya kuandika kabla ya kufanya matumizi na baada ya kufanya matumizi. Unapoenda kufanya matumizi ufanye kulingana na vitu ambavyo uliorodhesha katika karatasi yako. Hata kama kuna kitu utakipenda ukiwa katika matumizi ni muhimu kuzingatia vitu ambavyo ulipanga kununua tu. Hii itakusaidia kudhibiti matumizi yasiyo ya muhimu na nidhamu ya pesa.

d) Pendelea kununua vitu katika maduka ya jumla na uombe punguzo
Katika maduka ya jumla huwa bidhaa zinauzwa bei ya chini ukilinganisha na maduka ya reja reja, kwa hiyo kwa kufanya manunuzi katika maduka ya jumla inakusaidia kupata punguzo la bidhaa na kuokoa pesa. Ukifanya manunuzi pia uwe unaomba punguzo au kununua bidhaa ambazo zipo katika punguzo. Pesa zote ambazo utaokoa kwa kununua katika bei ya chini ni muhimu ukaziweka katika akaunti ya akiba.

e) Punguza au acha baadhi ya tabia au mazoea
Baadhi ya tabia ambazo tunazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na matumizi makubwa toka katika kipato ambacho tunakipata tabia hizo kama ulevi,uvutaji n.k. Ikiwa tutaweza kupunguza au kuacha kabisa basi hiyo pesa inatakiwa iingie katika akaunti ya akiba. Usije ukaacha baadhi ya tabia na hiyo pesa ukaipeleka katika jambo lingine ambalo halina faida yoyote.

f) Nunua nguo kwa ratiba
Uwe na ratiba maalumu ya kununua nguo na sio kila ukiona nguo nzuri ukiwa barabarani unanunua. Ili kulinda pesa zako ni muhimu kuwa na ratiba ya kununua nguo mara moja kwa mwezi au kununua kila baada ya miezi miwili na hii itasaidia kupunguza gharama zisizo za lazima na kukuondoa kwenye madeni.

g) Amua sasa kulipa madeni kwa awamu na kuacha kukopa bila sababu maalumu
Ikiwa una madeni ambayo bado una daiwa ni muhimu kulipa ili uweze kujenga uaminifu kwa watu. Ongea na muhusika ambaye ana kudai na mueleze kuwa una mpango wa kupunguza deni ambalo anakudai kila mwezi. Ila kumbuka kuweka akiba ya asilimia kumi na ndipo ufanye matumizi mengine kama kulipa madeni.

Natumai makala hii imeongeza elimu ya pesa kwako mdau wa mtandao huu, endelea kutembelea mtandao huu na kupata huduma zingine ambazo zitakusaidia katika kufikisha malengo yako ya kukuza kipato.

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi

GH

Tuesday, 12 February 2019

Ujumbe: Kwanini usinunue Hisa Zinazouzwa Bei Ndogo

Habari ndugu msomaji wa Mtandao huu wa Wekeza Mtanzania karibu tena katika safari ya kuongeza maarifa kuhusu uwekezaji na uhuru wa kifedha, na uwekezaji katika Hisa. Leo ni siku nyingine napenda kukushirikisha kanuni na sheria mojawapo unapohitaji kununua hisa kwenye kampuni yoyote.Kwanini usinunue hisa kwenye kampuni ambayo hisa zake zinauzwa bei ndogo
Watu wengi wamekuwa na tabia ya kufanya biashara kama vile biashara ya mazao ya nafaka na biashara zingine. Biashara hizi wamekuwa na tabia ya kununua mazao kama mahindi na maharage na kuyaifadhi ili wayauze baada yamuda fulani. Na mazao haya wamekuwa wakinunua katika bei ndogo na kuyauza kwa bei kubwa baada ya muda fulani.

Soma na hii Nunua Hisa kwenye Kampuni Hizi

Ila nakushauri ndugu mwekezaji katika hisa, usinunue hisa kwenye kampuni ambayo inauza bei ndogo. Bei ndogo ya hisa ya kampuni yoyote isiwe kigezo cha kuwekeza kwenye kampuni hiyo kwa leongo la kutengeneza faida kubwa katika kipindi kijacho. Wekeza kwa kununua hisa kwenye kampuni kwa sababu tu inafanya vizuri katika utendaji wake na inafanya vizuri katika soko la hisa.

Soma na Hii Taarifa ya fedha ya DSE ya Robo Mwaka 2018

Asante ndugu mwekezaji natumai utafanyia kazi na kuwekeza pesa yako sehemu salama na lengo la kukuza uwekezaji wako na kuongeza kipato likatimia.

Siku njema!!!!


Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi
GH

Sunday, 10 February 2019

Nunua Hisa kwenye Kampuni Hizi

Habari ndugu msomaji wa makala hizi za Wekeza Mtanzania, karibu tena upate kuongeza maarifa sahihi kuhusu uwekezaji katika hisa. Ndugu msomaji umeshaanza kuwekeza katika hisa? Ikiwa umeanza kuwekeza ' Hongera Sana'. Kama bado haujaanza kuwekeza katika hisa nakushauri uanze sasa. Na ikiwa haujui uanzie wapi Nitafute kwa namba hapo chini mwisho wa makala hii nikuelekeze.

Nunua hisa


Karibu katika makala ya leo tutadodosa kuhusu ni kampuni gani amabazo unaweza kuanza kuwekeza katika hisa na kujenga uwekezaji imara na wenye manufaa kwako mwekezaji. Kampuni ambazo zipo katika soko la hisa zinatofautiana ubora kutoka kampuni moja hadi nyingine. Kwa hiyo kazi yako mwekezaji ni kuchagua kampuni bora kuwekeza na kuendelea kujenga uwekezaji wako huku ukiwa unaendelea kupata gawio.

Baadhi ya wawekezaji wanapenda kununua hisa kwenye kampuni ambazo thamani yake ni sawa na thamani ambayo ipo sokoni. Baadhi ya wawekezaji upendelea kununua hisa kwenye kampuni ambazo bei zake zipo chini ya samani halisi ya kampuni (Mfano hisa za kampuni sokoni zinauzwa Shilingi 1000 ila thamani halisi ya hisa ni shilingi 2500), mwekezaji atanunua akiwa na lengo kuwa bei zitaongezeka kufikia thamani halisi. Ila mimi nakushauri ununue kwenye kampuni ambazo zinakua na ambazo bei ya sokoni ina akisi thamani ya hisa ya kampuni husika. 

Siku ya keo ndugu msomaji mpendwa nitakujuza sifa nzuri za Kampuni ambazo unatakiwa uweke mtaji wako (kununua hisa) ili uweze kufanya uwekezaji mzuri.

Chagua Kampuni ya kuwekeza katika Sekta zinazofanya vizuri. Mwekezaji unapotoa mtaji wako na kuwekeza lengo ni kukuza mtaji ili uweze kujitengenezea faida. Na ili uweze kutengeneza faida katika uwekezaji katika soko La hisa, ni muhimu kwako kuwekeza katika sekta ambazo zinafanya vizuri sokoni. Na utajuaje sekta Huduma au viwanda inafanya vizuri, ni kwa kupitia kusoma taarifa za kampuni pia na ufanisi wa kampuni hizo katika soko la hisa na kupata taarifa kuhsu utendaji wa kampuni husika.

Sekta ya Viwanda, Uwekezaji na Sekta ya Mabenki na Fedha, ndizo zinafanya vizuri sokoni (Katika soko la hisa la Dar es salaam) ukilinganisha na sekta nyingine. Pamoja kwamba nimeeleza kuwa sekta hizo zinafanya vizuri sio makampuni yote katika hizo sekta yanafanya vizuri. Kama mwekezaji unatakiwa kufanya uchunguzi kwa kila sekta ili uweze kuchagua kampuni nzuri ya kuwekeza ili kukuza uwekezaji wako.

Kwa kusoma taarifa za fedha za kampuni na kufuatilia mafanikio ya kampuni husika sokoni, Itakusaidia kuchagua kampuni nzuri. Kama nilivyoeleza mwanzo kuwa wekeza katika sekta inayofanya vizuri, na katika kila sekta chagua kampuni ambazo zinafanya vizuri katika sekta husika (Unachagua bora zaidi katika sekta hiyo) ili kufanya uwekezaji bora.

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi
GH

Thursday, 7 February 2019

Taarifa ya Fedha DSE ya Robo ya mwisho ya mwaka 2018 (Quarter 4)

Habari ndugu mwekezaji na mdau wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania, karibu tena katika mfululizo wa makala na taarifa ambazo zitaongeza ujuzi na kukupatia nafasi nzuri ya kufanikiwa katika uwekezaji katika hisa.

Taarifa ya Robo mwaka DSE


Leo nina habari njema kwako mwekezaji kukupatia uchambuzi kuhusu Kampuni ya Dar es slaam Stock Exchange (DSE) ambayo pia ipo katika soko la hisa. Taarifa hizi zinahusu kuhusu utendaji wake katika kujiingizia kipato, Matumizi, Faida na kuhusu gawio.

Nitaeleza kwa uchache ila katika vipengele muhimu ambavyo vitakupa mwanga kuhusu utendaji wa Kampuni hii ambayo ndiyo inahusika katika kusimamia shughuli zote za ununuaji na uuzaji wa hisa, pia ndio inayozisajili kampuni katika soko.


Uchambuzi wa Kampuni ya Dar es salaam Sock Exchange (DSE) katika Vipengele

1. Mapato (Revenue)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa disemba 2018 Kampuni ya DSE imeweza kutengeneza mapato ya bilioni (1,529,451,170) ukilinganisha na mapato ambayo ilitengeneza katika robo ya tatu ya septemba mwaka 2018 kwa kiasi cha shilingi bilioni (1,319,392,701). Mapato ya robo ya nne mwezi disemba yameongezeka kwa zaidi ya milioni mia mbili, sawa na asilimia kumi na tano (15.92%). Na hii ni ishara nzuri katika utendaji wa kampuni.

Kwanini Kampuni inauza Hisa Zake

2. Faida Baada ya Kodi (Profit after tax)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa disemba 2018, Kampuni ya DSE imeweza kutengeneza kiasi cha faida ya shilingi milioni mia tatu (307,729,168) ukilinganisha na faida ambayo ilitengeneza katika robo ya tatu ya septemba mwaka 2018 kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja (134,698,081). Faida ya robo ya nne ya mwezi disemba imeongezeka kwa zaidi ya milioni mia moja na sabini, sawa na ongezeko la faida kwa asilimia 128.5% kutoka kwenye faida ya robo mwaka ya tatu.

3. Kipato cha Kila Hisa (Earning per Share)
Katika taarifa ya robo mwaka wa mwisho wa mwezi disemba 2018, kampuni imeweza kutengeneza mapato ya kila hisa moja ya shilingi 13 ukilinganisha na mapato ya robo ya tatu mwaka 2018 ya shilingi 6 kwa kila hisa moja. Katika robo mwaka wa nne mapato kwa kila hisa yameongezeka kwa kiasi kikubwa sawa na asilimia 116.7% toka kwenye mapato kwa kila hisa ya robo tatu ya mwaka 2018.

Zingatia haya unapoanza Kuwekeza katika Hisa

Ili kuweza kusoma taarifa nzima ya robo ya nne ya mwaka 2018 bonyeza maandishi hapo chini na kuweza kupakua taarifa nzima.

Pakua taarifa na Kuisoma kwa kubonyeza linki hii
Link Download Unaudited financial statement quarter ended december

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
MwandishiGH

Monday, 4 February 2019

Ujumbe wa Leo: Niwekeze kwenye Kampuni Ngapi??

Habari ya siku nyingine ndugu mwekezaji na msomaji wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania. Karibu katika siku nyingine kwa ajili ya kuongeza maarifa katika nyanja ya uwekezaji katika hisa za kampuni zilizo katika soko la hisa (Soko la Hisa la Dar es Salaam).

Kampuni ya kuwekeza


Katika Ujumbe wa leo kwako mwekezaji na msomaji wa mtandao huu, Napenda kuzungumzia kuhusu ni kampuni ngapi unashauri kuwekeza.

Wekeza kwenye Kampuni kubwa na chache, Muhimu kuchagua kampuni kubwa na mara zote kampuni kubwa ndio ambazo zinafanya vizuri. Kampuni kubwa ni ile ambayo inafanya mauzo mazuri, Faida inayoongezeka kila mwaka kwa 20% au zaidi. Katika Kampuni kubwa chagua kampuni tatu hadi sita, ila inategemea kiasi cha mtaji ambacho unacho katika kipindi hicho. Ni muhimu kuwekeza katika hiyo idadi ya kampuni ili iwe rahisi kufuatilia uwekezaji wako ili uweze kutengeneza faida nzuri.

Soma... Kwanini Kampuni inauza hisa zake

Kuna usemi unasema " Unalipwa kutokana na kiasi ambacho umetoa" Katika uwekezaji katika Hisa utalipwa kulingana na thamani unayotoa unapofanya uwekezaji wako. Ukinunua hisa kwa sababu zinauzwa bei ndogo, vile vile utalipwa kwa thamani ndogo au kupoteza kabisa mtaji. Mara zote kampuni kubwa ndizo ambazo zinafanya vizuri sokoni na ndizo ambazo bei zake zipo chini. Kwa hiyo ndugu mwekezaji nakushauri wekeza kwenye Kampuni kubwa na ambayo inafanya vizuri sokoni na katika utendaji wake. Usishawishiwe kununua hisa kwenye kampuni kisa inauzwa katika bei za chini.

Jinsi ambavyo utafanikiwa katika uwekezaji

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
Mwandishi
GH

Sunday, 3 February 2019

Kwanini Kampuni Inauza Hisa zake

Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania, karibu katika mfululizo wa makala za kuhamasisha na kuelimisha kuhusu uwekezaji katika hisa na kuongeza kipato. Asante Mungu kwa siku nyingine, nawakaribisha katika kuongeza maarifa katika kukuza kipato na uhuru wa kifedha.

Kampuni Kuuza hisa 


Karibu katika makala ya leo kuhusu kufahamu sababu za kampuni kuuza hisa zake kwa wakezaji. unaweza kuona kama, makala hii haikugusi moja kwa moja ila nakusihi uendelee kusoma kwa sababu utakachojifunza kitakusaidia katika maisha yako ya kawaida katika biashara zako.

Maisha katika biashara na uwekezaji ni kama ukuaji wa mtoto. Ukuaji wa mtoto una hatua mbalimbali kutoka kuzaliwa kwake na ukuaji wake una changamoto na mifumo ya mabadiliko.
Hata kampuni zinapoanzishwa zinapitia hatua ndogo ndogo hadi kufikia kuitwa kampuni kubwa. Kampuni ina anza na watu wachache ila kila inavyoendelea kukua umiliki na uendeshaji wake unazidi kuongezeka. Na hii ndio njia abayo kampuni ndogo zinapitia hadi kufikia kuwa kampuni kubwa.Kampuni ina machaguo kati ya kukopa au kupata fedha toka kwa mwekezaji inategemea aina ya mradi na kiasi cha fedha ambacho kinahitaji.

Siku za hivi karibuni nilikutana na rafiki yangu ambaye baada ya kuongea mambo mengi toka tulipoacha tukiwa shule alitaka nimuelezee, Kwanini kampuni inauza hisa? Bila kuwa mchonyo nikaona ni vyema nikawashirikisha ndugu wasomaji wa mtandao huu ili na nyinyi mpate kujua machache kuhusu sababu za Kampuni kuuuza hisa zake.

Kampuni inapohitaji kufanya mradi mkubwa ina maamuzi mawili kukopa toka taasisi za fedha kama benki au kupata mtaji toka kwa wawekezaji ambao watakuwa tayari kuweka mtaji wao katika mradi wa kampuni. Na wawekezaji wakitoa pesa katika kampuni husika katika mfumo wa kununua hisa na wao wanakuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni.

umuhimu-wa-mwanafunzi-wa-chuo kujijengea nidhamu ya kuweka akiba

Kuna Mfano mdogo ambao utakupa mwanga kwanini Kampuni zinauza hisa katika jamii na wanauzaje?? Mfano huu unahusu mjadiliano ambayo nilifanya na rafiki yangu ambaye alihitaji nimueleze kwanini Kampuni zinauza hisa. Majadiliano yalikuwa hivi

"Nikamwambia kwa mfano Mimi nataka kufungua Duka pale mtaani kwetu"

Akashangaa "eeeh unataka kufungua Duka" Nikamwambia huu  ni mfano tu.

Mfano Nahitaji kufungua duka, mtaji WA bidhaa na gharama za chumba ni Milioni moja,  ila mimi nina laki tisa tu. Nakuomba uniongezee laki moja kwa makubaliano ya kuwa mmiliki wa duka kwa asilimia kumi (10%).

Soma na hi Tafsiri rahisi nini Maana ya Hisa

"Kwa kukubali kutoa shilingi laki moja kwenye mtaji wa duka,  na wewe unakuwa mmiliki wa duka kwa asilimia kumi" Nilimuambia rafiki.

Baada ya mwaka duka likatengeneza faida ya Laki tano, kwa kuwa rafiki yangu wewe ni mmiliki kwa asilimia kumi utapata faida ya shilingi elfu hamsini (Gawio) kama sehemu ya kumi ya faida ya duka.

Baada ya miaka miwili Duka likatengeneza faida nzuri,  tukaona kuna uhitaji wa kufungua Duka jingine lenye mtaji wa milioni moja.

Nikamuuliza Rafiki " Baada ya kufungua Duka la pili,  jumla tuna mtaji wa Shilingi Ngapi?
Akajibu "Milioni mbili"

Kumbuka Rafiki " Mwanzo ulitoa laki moja kama mtaji Na ukawa mmiliki wa Duka kwa asilimia 10%, Na Baada ya miaka miwili duka limekua na kuweza kufungua Duka la pili na mtaji umeongezeka  na kufikia milioni Mbili. Kwa maana hiyo baada ya biashara ya Duka kukua na mtaji wako unakua kutoka laki moja hadi laki Mbili. Hii inaitwa ongezeko la thamani ya umiliki wako (Capital appreciation).

Na ikiwa mtu mwingine akihitaji kukulipa kiasi ambacho unamiliki utakubali Rafiki??  Nikamuuliza
Akajibu Ikiwa mtu atahitaji kuchukua umiliki wangu katika Duka nitamuuzia kwa  laki mbili.

Nikamuuliza kwanini laki mbili Akajibu kwa sababu thamani ya umiliki wangu umeongezeka baada ya duka kutengeneza faida nzuri na kuweza kufungua duka la pili. Jumla ya maduka yote yana mtaji wa milioni mbili na mimi namiliki asilimia kumi ya biashara ya duka (10%).

Na ikiwa watakuja watu watatu wanahitaji uwauzie Akajibu Ikiwa watakuja watu watatu au zaidi wakitaka umiliki wangu nitawauzia kwa laki tatu au zaidi.

Kwanini rafiki yangu yupo tayari kuuza zaidi thamani halisi, kwa sababu anafahamu kuwa umiliki wake una thamani na thamani itaendelea kuongezeka zaidi Baada ya kuona Duka linafanya vizuri na uwezekano wa kufanya vizuri zaidi. Vile vile imekuwa rahisi kwake kuongeza bei za hisa zake za duka baada ya kuona uhitaji umeongezeka. Hapo Rafiki ameweza kuona thamani ya sasa (Current value) na anamatarajio ya thamani kuongezeka zaidi (Expected Value).

Kwa huo mfano rahisi kabisa, unaweza kutambua ni kwanini kampuni zinauza hisa zake. Kampuni inauza hisa kwa sababu;

Wanahitaji mtaji, Mtaji kwa ajili kufanya miradi mikubwa ya kampuni ambayo ina malengo ya kupanua wigo wa biashara, kununua mashine za kisasa au kuongeza ufanisi wa Kampuni ili iweze kutengeneza faida maradufu. Na njia yenye gharama nafuu na kuuza hisa katika jamii na jamii kuwa sehemu ya wamiliki katika hisa.

Kujulika, Kampuni ukishauza hisa zake kwa umma ni njia mojawapo ya kujulikana kwa watu wengi. Kwa sababu ni rahisi kusambaa taarifa zake kwa watu wengi zaidi, ila itakuwa mbaya ikiwa kampuni itafanya vibaya sokoni.

Mwekezaji akinunua hisa atanufaika kwa;

Ongezeko la bei (Capital appreciation) Kama ambavyo tumeona katika mfano hapo juu thamani ya hisa ikiongezeka na mtaji unaongezeka pia. Na hii uchangiwa na kufanya vizuri kwa kampuni na matarajio ya mwekezaji katika kipindi kijacho.

Gawio (Dividend) Jinsi ambavyo kampuni inatengeneza faida ndivyo mwekezaji anavyokuwa na uhakika wa kupata gawio la kutosha.

Asante ndugu msomaji wa mtandao, nakusihi endelea kutembelea mtandao wetu wa Wekeza Mtanzania kwa mafunzo zaidi ili kufikia uhuru wa kifedha kwa kuwekeza katika hisa (Soko la Hisa)

Kwa ushauri au maelezo zaidi tuwasiliane kwa namba 0714 445510 ila unatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 10,000/=.

KARIBU SANA

Emmanuel Mahundi
MwandishiGH

Wednesday, 30 January 2019

Ujumbe: Wekeza kwenye Kampuni Kubwa

Habari ndugu msomaji wa mtandao huu wa Wekeza Mtanzania, karibu tena katika siku nyingine katika safari ya kuongeza maarifa ili kuweza kufanya uwekezaji bora na kuongeza kipato. Katika siku ya leo nina ujumbe kwako mwekezaji katika hisa kuhusu kuchagua kampuni ya kuwekeza. Na kama bado haujanza kuwekeza nakushauri uanze mapema ili uanze kuongeza thamani ya uwekezaji wako.

Wekeza kwenye Kampuni kubwa


Kama nilivyoeleza hapo juu, leo nitazungumzia kuhusu kuchagua kampuni ya kuwekeza katika soko la hisa. Katika soko kuna Kmapuni zaidi ya ishiri, na kampuni zote zinauzwa bei tofauti vile vile zina thamani tofauti.

Ushauri wangu kwako mwekezaji kabla haujanunua hisa zingatia haya machache kuhusu kuwekeza katika hisa;

Usinunue hisa kwa sababu zinauzwa bei ndogo
Ndugu mwekezaji unapohitaji kununua hisa, usiangalie kwa sababu kampuni inauza hisa zake katika bei ndogo ambayo itakufanya upate hisa nyingi. Utapoteza mtaji wako ikiwa utazingatia udogo wa bei iliyo sokoni. Nunua hisa kwenye kampuni Kubwa na mara nyingi zinauzwa katika bei kubwa, ila sio kampuni zote zenye bei kubwa ni nzuri.

Zingatia haya unapoanza kuwekeza katika hisa

Kampuni kubwa ina sifa zifuatazo ndugu msomaji/mwekezaji Ina mauzo mazuri ya bidhaa/huduma, Inatengeneza faida nzuri, Inatoa gawio wa wawekezaji, Ina uongozi mzuri na mipango mizuri ya bidhaa/huduma zake katika kipindi kijacho. Kwa kifupi ni kampuni ambayo inajiendesha kwa kutengeneza faida na pia inafanya vizuri sokoni (Soko la Hisa).

Soma hii.. Jinsi ya kuchagua Uwekezaji unaokua

Natumai kwa haya machache umefahamu kuhusu utaratibu mzuri wa kuchagua kampuni unapohitaji kuwekeza katika hisa.

Asante na endelea kutembele mtandao huu usisahu kulike ukurasa wetu wa Facebook na kupakua app kwenye matangazo ya pembeni.

Kazi Njema

Kwa ushauri au ufafanuzi zaidi tuwasiliane kwa 0714 445510 ila utachangia shilingi 10,000 kwa tigo pesa.

Emmanuel MahundiGH

Tuesday, 29 January 2019

Zingatia haya Unapoanza Kuwekeza katika Hisa

Habari ndugu msomaji wa mtanadao huu wa Wekeza Mtanzania. Tunasema asante mungu kwa siku nyingine, vile vile asante ndugu msomaji kwa kuendelea kutembelea mtandao huu. Bila wewe msomaji sisi hatuna cha kujivunia katika kazi yetu ya uandishi.

Zingatia haya unapoanza kuwekeza 


Karibu tena ndugu msomaji katika somo letu la leo kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanya uwekezaji katika hisa.. Ni muhimu kupata kuyafahamu mambo muhimu na ya msingi ili safari ya mafanikio na uhuru wa kifedha iwe ya uhakika na yenye mafanikio makubwa.

Nipende kukumbusha kuwa kabla hatujaangalia mambo muhimu kuzingatia katika safari ya kuanza kuwekeza ni muhimu ukaweka malengo ya muda mrefu ili kufikia uhuru wa kifedha wa uhakika. Na kama haujaanza kuwekeza katika hisa, nakushauri uanze sasa, huu ndio uwekezaji ambao utakuhakikisshia kipatoa cha uhakika baada ya nguvu ulizonazo leo kupungua, na ndio uwekezaji ambao unakupa uhuru wa kufanya shughuli nyingine bila usimamizi wa karibu sana.

unataka-kuwekeza-katika-hisa-soko-la hisa na haujui uanzie wapi

Mambo haya muhimu kuzingatia unapoanza safari kuwekeza katika hisa

1. Chagua mshauri atakayekuongoza
Ukitaka kufanya jambo lolote kwa ubora na matokeo mazuri, Ni muhimu ukachugua mtu wa kukuongoza ambaye ameshafanya Fanya jambo hilo kwa ubora au mwenye taaluma husika. Kabla ya kuanza uwekezaji wako ni vyema ukachagua mshauri ambaye ni mtandao huu wa uwekezaji na Mtanzania kwa kusoma makala zetu, na ikiwa utahitaji ushauri zaidi toka kwa mwandishi unakaribishwa ila kwa Malipo. 

2. Fuatilia uwekezaji wako
Uwekezaji katika hisa unahitaji ufuatiliaji Kama biashara nyingine hasa kuangalia mwenendo wa bei na ufanyaji kazi wa kampuni ambazo umewekeza. Hii inakusaidia kujua kampuni ambazo umewekeza ambazo zinafanya vizur sokoni. Na pia itakusaidia kujua ni muda sahihi wa kuuza au kununua hisa katika soko.

faida-aipatayo-mwekezaji-kuwekeza katika Hisa

3. Uwekezaji upi wa kuepuka
Kama mwekezaji unatakiwa kuwa na tahadhari ili kupunguza hatari ya kupoteza pesa yako ukiwa unafanya uwekezaji katika hisa. Hatari mojawapo ya kuzingatia hasa unapochagua kampuni ya kuwekeza, usichague kampuni kwa sababu sokoni hisa zake zinauzwa bei ya chini. Nunua hisa kwenye kampuni ambayo ina rekodi nzuri ya mapato, Faida na yenye malengo mazuri. 

4. Kiasi gani cha pesa kinahitajika ili uanze kuwekeza
Watu wengi wakisikia kuhusu uwekezaji, mawazo yao wanahisi inahitajika kiasi kikubwa cha pesa ili uanze kuwekeza katika hisa. Kuwekeza katika hisa hauhitaji pesa nyingi ili uanze kuwekeza, utahitaji kiasi cha shilingi 30,000/= tu au zaidi na utaanza kuwekeza katika soko la hisa na kuanza kuwa mmiliki wa baadhi ya kampuni. Unahitaji kuwa na subira na kuwa na utaratibu wa kununua hisa mara kwa Mara. Ikiwa utakuwa na mtaji wa shilingi 30,000/= hadi 200,000/= nunua hisa kwenye kampuni moja utaongeza uwekezaji wako kwenye kampuni nyingine.  Na ikiwa una mtaji wa shilingi 500,000/= au zaidi wekeza kwenye kampuni mbili au zaidi katika kampuni tofauti.

umuhimu-wa-mwanafunzi-wa-chuo kujijengea nidhamu ya kuweka akiba

5. Umiliki hisa katika Makampuni mngapi
Katika soko la hisa unaruhusiwa kuwekeza katika Kampuni zaidi ya moja. Muhimu kuchagua kampuni ambazo zinafanya vizuri katika mauzo, faida na katika soko. Kwa kuanza nakushauri uanze kuwekeza kwenye tatu, baada ya kufahamu mambo mengi zaidi katika uwekezaji unaweza kuongeza kampuni zaidi za kuwekeza. Ila kumbuka kuzingatia na kiasi cha mtaji ambacho unacho Kama nilivyoelekeza katika maelezo hapo juu. 

6. Vitabu gani muhimu kusoma
Mafanikio = Maarifa sahihi +Muda + Uvumilivu. Ili uweze kufanikiwa katika uwekezaji au katika jambo lolote ni muhimu ukawa na maarifa na taarifa sahihi ambazo zitakusaidia katika kufanya maamuzi sahihi. Kama ni msomaji wa makala katika mtandao huu wa uwekezaji na mtanzania natumai unapata maarifa sahihi ya kukuwezesha kufanya uwekezaji ulio mzuri, ila unaweza kuongeza ujuzi zaidi kwa kusoma vitabu, majarida na nakala zozote ambazo zitaongeza zaidi uelewa wako katika kuwekeza katika hisa. 

7. Zingatia kuwekeza katika Kampuni bora usiwekeze kwenye Kampuni nyingi
Unaweza kufikiri kuwekeza au kununua hisa kwenye kampuni nyingi ndio itakusaidia kufanya vizuri. Unatakiwa kuchagua kampuni bora ambazo zinafanya vizuri sokoni kuliko zingine na sio kuwekeza katika kampuni nyingi. Unaweza kuwekeza tano au tatu tofauti na ukajenga uwekezaji ulio Nora zaidi. 

Nikutakie wakati mwema, na kukaribisha kuendelea kujifunza zaidi kupitia makala zangu

Ukihitaji Ushauri au Maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana kwa Namba 0714 445510 Ila kwa malipo ya shilingi 10,000/=

Emmanuel Mahundi
GH

Thursday, 25 January 2018

Unataka Kuwekeza Katika Hisa (Soko la Hisa) na haujui uanzie wapi ??

Karibu ndugu wasomaji wa mtandao huu wa uwekezaji na Mtanzania katika mfululizo wa makala za kukuelimisha na kukuabarisha kuhusu uwekezaji katika hisa.

Unataka Kuwekeza haujui uanzie wapi


Je umekuwa ukisikia kuhusu soko la hisa na uwekezaji katika soko la hisa na unapata shida ni wapi utaanzia. Haujui ni wapi utaanzia Jinsi gani utawekeza Kampuni gani nzuri ya kuwekeza ? Ikiwa umekuwa na shahuku kubwa ya kupata majibu ya maswali yote hayo kuhusu uwekezaji katika soko la hisa basi upo sehemu sahihi ya kupata majibu.

Haujui wapi utaanzia Jinsi gani utawekeza

Kama unataka kuwekeza na haujui wapi utaanzia ili uweze kuwa mmiliki wa hisa katika kampuni tofauti. Kuna jarida ambalo limeandaliwa kukupatia mwongozo ambao utakusaidia hatua za mwanzo hadi mwisho na kuweza kununua hisa. Kwanini nimeandaa jarida hili ?  Nimekuwa napokea simu na email nyingi za wasomaji kayika blogu www.wekezamtanzania.blogspot.com wakitaka kupata mwongozo jinsi gani wanaweza kununua hisa kwa Kampuni ambazo zipo katika Soko la Hisa.

Mwongozo huu utakusaidia kufahamu taratibu za kununua hisa katika soko la awali na katika soki la hisa na vitu vya muhimh kuwa navyo ili kukamilisha taratibu za ununuzi.

Kupata Mwongozo huu, tuma fedha shilingi 4,000 kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako kisha nitakutumia mwongozo huo kwenye email yako.

Kampuni gani nzuri ya kuwekeza ?

Umekuwa ba shahuku ya kutaka kuwekeza katika kampuni zilizo katika soko la hisa ila haujui una anzia wapi na Kampuni ipi ni nzuri kwa ajili ya kukuza uwekezaji wako. Basi tumekuandalia uchambuzi taarifa za Kampuni ambazo zipo katika Soko la Hisa. Uchambuzi huu utakusaidia kufahamu ufanisi wa Kampuni kutokana na taarifa zao za fedha na wewe kuweza kufanya uchaguzi sahihi wa Kampuni ya kuwekeza.

Jinsi ambavyo utafanikiwa katika Uwekezaji

Uchambuzi huu umechambua Kampuni katika sekta tofauti na wewe kujua ni Kampuni ipi katika kila sekta inafanya vizuri kulingana na taarifa zao za fedha.

Uchambuzi huu umeangalia kwa kiasi kikubwa Kampuni inatengeneza faida kwa kiasi gani, Kwa kiasi gani kampuni inatumia vyema rasilimali zake, Uwezo wa Kampuni kulipa madeni na kuondoa hatari ya kufilisika, Uwezo wa rasilimali kuzalisha faida ya kutosha  na Utambuzi wa hatari na fursa mbalimbali za kampuni katika mazingira ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ili uweze kufanya uwekezaji wenye manufaa kwako katika kipindi kirefu.

Uchambuzi huu utakuwa unapatikana katika sekta, yaani kila sekta Kampuni zimechambuliwa na kupendekeza ni kampuni zipi nzuri zaidi kwa uwekezaji. Tumegawa katika sekta ya Huduma (Commercial services), Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji (Finance, Banking and Investment), Sekta ya Viwanda (Industrial), Sekta ya Madini (Mining) na Mawasiliano (Telecom).

Kupata Uchambuzi huu,

Sekta ya Huduma kwa Shilingi 10,000

Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji Shilingi 10,000

Sekta ya Viwanda kwa Shilingi 10,000

Sekta ya Madini na Mawasiliano kwa pamoja unapata kwa Shilingi 10,000

Ikiwa utahitaji kupata Uchambuzi kwa sekta zote kwa Pamoja utalipia Shilingi 30,000 badala ya kulipia shilingi 40,000.

Malipo unafanya kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako kisha utachagua uchambuzi katika sekta moja au zaidi, baada ya hapo nitakutumia kwenye email yako.

Emmanuel Mahundi
emmanuelmahundi@gmail.com
GH

Tuesday, 23 January 2018

HISA: Jinsi ambavyo Utafanikiwa katika Uwekezaji

Hakuna jambo gumu ambalo wawekezaji wengi wanakutana nalo kama kuchagua uwekezaji wa kampuni ambayo inafanya vizuri na itaendelea kufanya vizuri. Na hiki ni kitu muhimu kwa mwekezaji kwa sababu lengo kubwa la mwekezaji ni kuongeza thamani ya uwekezaji wake.

Jinsi ambavyo Utafanikiwa katika Uwekezaji 


Jambo muhimu kwa mwekezaji anapoamua kuwekeza katika hisa ni muhimu kutoendeshwa na hisia katika maamuzi ya kununua na kuuza hisa. Kwa sababu unaweza kuuza hisa zako kwa sababu tu hisa zako zimeshuka kwa asilimia 10% katika kipindi fulani. Kumbe kushuka kwa hisa zako ni mzunguko tu wa muda hasa pale taasisi kubwa zinapouza hisa kwa wingi katika soko.

Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kusababisha kushindwa kufanikiwa katika uwekezaji wa hisa ila muhimu kufahamu vitu hivi ambavyo vitaongeza nafasi ya ushindi katika uwekezaji wako katika soko la hisa


Kupata Pesa nyingi ni Muhimu ukanunua hisa katika Kampuni bora na katika kipindi sahihi

Ili mwekezaji uweze kutengeneza pesa nyingi katika uwekezaji wako ni muhimu kununua hisa katika kampuni bora. Kampuni bora ni kampuni ambayo inafanya vizuri katikauendeshaji wake na vile vile inamatarijio ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Unawezaje kujua kampuni hii ni bora

Tunafahamu kampuni bora toka katika taarifa zake za fedha kwa kufanya uchambuzi wa taarifa za fedha za Kampuni (Tuna angalia mauzo ya kampuni, Faida ya kampuni, uwezo wa kutumia rasilimali za kampuni n.k)

Ni muhimu kununua hisa kwenye kampuni bora katika kipindi sahihi, mfano kipindi ambacho kampuni inauza hisa zake kwa mara kwanza (IPO) hapa mara nyingi hisa huuuzwa chini ya thamani hali ya kampuni kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji.
 Angalizo usinunue hisa kwa kila kampuni ambayo inauzwa hisa zake kwa mara ya kwanza, muhimu kusoma taarifa muhimu za kampuni kabla ya kununua hisa.

Angalia kampuni ambayo ina mauzo makubwa (sales) na mapato kwa mwekezaji ni makubwa (earnings per share)

Mauzo ya Kampuni ni kipimo cha kampuni katika kufanya vizuri katika soko na sekta husika. Utatambua mauzo ya kampuni kwa kusoma katika taarifa za fedha za kampuni husika na kujua kwa kiwango gani kampuni imeweza kupata mauzo ya kutosha. Hata kwa biashara ndogo, ikiwa biashara ina mauzo makubwa ni kipimo cha kuonyesha biashara hiyo ina mzunguko mkubwa katika soko.

Kama mwekezaji ni muhimu kuangalia kampuni yenye mauzo makubwa na ambayo ina kipato zaidi kwa wawekezaji (EPS). Kwa sababu kipato kwa mwekezaji ni kipimo cha kampuni kutengeneza faida ya kutosha kwa wawekezaji.


Angalia Kampuni ambayo inatoa mapato makubwa kwa wanahisa (ROE)

Kama ilivyo kwa mfanyabiashara atachagua biashara ambayo ana uhakika itampatia faida ya kutosha na kuweza kurudisha mtaji wake. Hata katika uwekezaji katika hisa ni muhimu kwa mwekezaji kuwekeza katika kampuni ambayo inatoa mapato makubwa kwa mwekezaji. Mapato hayo ndio kiashiria cha utumiaji vizuri wa rasilimali za kampuni, pia ndio mapato ambayo mwekezaji anapata baada ya pesa yake kuwekeza katika mtaji wa kampuni husika.

Kama unataka kuwekeza kwenye kampuni yoyote angali (ROE) ambayo ina anzia kwa asilimia 15% au zaidi ya hiyo.

KUPATA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA FEDHA ZA KAMPUNI 

Sekta ya Huduma (Commercial services) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Fedha, Benki na Uwekezaji (Finance, Banking and Investment) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Viwanda (Industrial) kwa Tsh 10,000
Sekta ya Madini (Mining) na Mawasiliano (Telecom) kwa pamoja unapata kwa Tsh 10,000

Ikiwa utahitaji kupata Uchambuzi kwa sekta zote kwa pamoja utalipia Tsh 30,000 badala ya kulipia Tsh 40,000.

Malipo unafanya kwa namba 0714 445510 (Jina Emmanuel Mahundi) kisha tuma ujumbe kwenye namba hiyo ukiambatanisha na email yako.

Angalia mzunguko wa bei katika soko

Ili mwekezaji inatakiwa kuwa makini katika kipindi cha kununua ili iweze kutengeneza faida ya kutosha katika hisa. Nunua hisa bei ikiwa katika ambacho ina anza kupanda, katika kipindi hiki mwekezaji anakuwa na uhakika wa uwekezaji wake kukua katika kipindi kifupi cha uwekezaji wake. Nawezaje kujua bei ina karibia kupanda ? Ili uweze kufanikiwa kwa kutumia mbinu hii unatakiwa kuwa na utamaduni wa kufuatilia mabadiliko ya bei kwa kampuni ambazo umechagua kuwekeza, katika kufuatilia mabadiliko hayo unaweza kujua bei zimeshuka na kwa muda huo zimeanza kuongezeka.

Asante kwa kuendelea kuwa Msomaji wa blog hii

Emmanuel Mahundi
emmanuelmahundi@gmail.com

GH